Tuesday, October 12, 2021

 


UFARANSA imetwaa ubingwa wa Ligi ya Mataifa ya Ulaya baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Hispania usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Giuseppe Meazza Jijini Milan, Italia.
Baada ya kipindi cha kwanza kumalizika bila mabao, dakika Mikel Oyarzabal alianza kuifungia Ufaransa dakika ya 64, kabla ya Karim Benzema kuisawazishia Ufaransa dakika moja baadaye na Kylian Mbappe kufunga la ushindi dakika ya 80.
Mapema jioni ya jana katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu, wenyeji Italia waliwachapa Ubelgiji 2-1 Uwanja wa Allianz Jijini Turin.
Mabao ya Italia yalifungwa na Nicolo Barella dakika ya 46 na Domenico Berardi kwa penalti dakika ya 65, wakati la Ubelgiji lilifungwa na Charles De Ketelaere dakika ya 86.

0 comments:

Post a Comment