Tuesday, October 12, 2021



 MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said Mohamed amesema kuwa kwa sasa mpango mkakati wao kama GSM ni kuhakikisha wanaimarisha kikosi cha Yanga ili kiwe imara kila idara kufanya vyema kwenye mashindano ya kimataifa msimu ujao.

Kwa sasa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi imeweka kambi Kigamboni katika kijiji cha Avic Town kwa ajili ya maandalizi ya mechi zijazo ndani ya ligi ambapo mchezo ujao itakuwa dhidi ya KMC, Uwanja wa Majimaji, Songea.

Kwa sasa imeelezwa kuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga ambaye ni raia wa Burundi, Said Ntibanzonkiza ‘Saido’ kuna uwezekano kwenye dirisha dogo la usajili ataachwa na mabosi wake hao.

Tetesi hizo zinadai kwamba nafasi yake inatajwa kuchukuliwa na mshambuliaji tegemeo kwa sasa wa timu ya taifa ya Uganda ambaye anakipiga katika Klabu ya FC Ashdod ya Ligi Kuu Israel.

Nyota huyo anaitwa Fahad Bayo ambaye alizaliwa 10 mei 1998 katika mji wa Lugazi Uganda ana urefu wa 1.85.

0 comments:

Post a Comment