Wednesday, January 26, 2022

 



MASHABIKI wa Simba SC wa tawi la Wekundu wa Chalinze wamepata ajali kijiji cha Wendele wilayani Kahama, mkoani Shinyanga mchana wa leo wakiwa njiani kuelekea Bukoba ambako timu yao kesho inacheza na wenyeji, Kagera Sugar.
Kikosi cha Simba kimewasili salama Bukoba mapema leo kwa ajili ya mchezo wake huo wa kiporo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Kagera Sugar kesho Saa 10:00 jioni Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

0 comments:

Post a Comment