Wednesday, January 26, 2022

 



MOROCCO imetoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Malawi katika mchezo wa Hatua ya 16 Bora Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika usiku huu Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaoundé nchini Cameroon.
Malawi ilitangulia kwa bao la mshambuliaji wa Orlando Pirates ya Afrika Kusini, Hellings Frank ‘
Gabadinho’ Mhango dakika ya saba, kabla ya mshambuliaji wa Sevilla ya Hispania, Youssef En-Nesyri kuisawazishia Morocco dakika ya 45 na ushei na beki wa Paris-Saint Germain, Achraf Hakimi Mouh kufunga la ushindi dakika ya 70 kuwapeleka Robo Fainali Simba wa Atlasi.

 Katika mchezo uliotangulia, Senegal ilikwenda Robo Fainali pia baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya  Cape Verde, mabao ya washambuliaji, Sadio Mané wa Liverpool dakika ya 63 na Cheikh Ahmadou Bamba Mbacke Dieng wa Marseille dakika ya 90 na ushei Uwanja wa Bafoussam.
Cape Verde ilicheza pungufu kwa muda mrefu, kufuatia wachezaji wake wawili kutolewa kwa kadi nyekundu,kiungo Patrick Andrade dakika ya 21 na kipa Josimar José Évora Dias  ‘Vózinha’ dakika ya 57.
Morocco itakutana na mshindi kati ya Ivory Coast na Misri na 
Senegal itakutana na mshindi kati ya Mali na Equatorial Guinea zinazokamilisha Hatua ya 16 Bora kesho.

0 comments:

Post a Comment