Wednesday, January 26, 2022

 

Luis Diaz

Ofa ya Tottenham ya takriban pauni milioni 38 kwa winga wa Porto kutoka Colombia Luis Diaz, 25 imekataliwa. (Guardian)

Aston Villa wanakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili kiungo wa kati wa Juventus na Uruguay Rodrigo Bentancur, 24. (Football Insider)

Newcastle haitamsajili mlinzi wa Brazil Diego Carlos kwani Sevilla wameamua kumbakisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Fabrizio Romano)

Rodrigo Bentancur

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Lakini Magpies wametoa ofa ya karibu pauni milioni 30 kwa kiungo wa Lyon na Brazil Bruno Guimaraes, 24. (Daily Mail).

Kiungo wa kati wa Paris St-Germain na Uholanzi Georginio Wijnaldum, 31, yuko tayari kuhamia Arsenal. (Sky Sports - kupitia Daily Mail)

Liverpool na Manchester City ndizo klabu zinazovutiwa zaidi kumsajili kiungo wa kati wa Leicester na Ubelgiji Youri Tielemans, 24. (Fichajes - kupitia Leicester Mercury)

Youri Tielemans

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Juventus wamefikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji Dusan Vlahovic kutoka Fiorentina, na hivyo kuzima matumaini yoyote ya Arsenal kumnasa mchezaji huyo wa kimataifa wa Serbia mwenye umri wa miaka 21 hadi Emirates. (Goal)

Everton wamejitokeza kutafuta saini ya kiungo wa kati wa Tottenham na Ufaransa Tanguy Ndombele, 25. (Sky Sports - kupitia TEAMtalk)

Brighton wanamfuatilia kiungo wa Tottenham Dele Alli kwa nia ya kumnunua kwa mkopo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 lakini Burnley, Everton na Newcastle pia wanahusishwa na Mwingereza huyo. (Mail)

Dele Alli

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Southampton pia wanafikiria kumnunua Alli. (Telegraph - kupitia Daily Echo)

Burnley wanakaribia kumsajili kiungo wa Dinamo Zagreb na Croatia Mislav Orsic, 29. ((Sky Sports)

Mshambulizi wa Everton Dominic Calvert-Lewin, 24, kiungo wa kati wa Wolves Ruben Neves, 24, na Douglas Luiz wa Aston Villa, 23, wako kwenye orodha ya kuhama iliyoandaliwa na meneja wa Arsenal Mikel Arteta.

Brentford wameongeza ofa yao kwa kiungo wa Nottingham Forest Brennan Johnson, ambaye pia anafuatiliwa na Newcastle. (Independent)

West Ham wanafikiria kumnunua mlinzi wa Croatia na Marseille Duje Caleta-Car, lakini wamezuiwa na bei ya pauni milioni 20 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Talksport)

AC Milan wanatafuta kumnunua mshambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang. Mshambulizi huyo wa Gabon mwenye umri wa miaka 32 anasemekana kukataa ofa ya Al-Nassr ya Saudi Arabia. (Football Italia)

Pierre-Emerick Aubameyang

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Newcastle itamkosa kiungo wa kati wa Atalanta Robin Gosens huku Juventus wakipania kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 27. (Goal)

Kipa wa Arsenal Bernd Leno, 29, anashinikiza kuondoka Emirates, huku Newcastle wakiwa na nia ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani kwa mkataba wa mkopo hadi mwisho wa msimu. (Football.london)

Red Bull Salzburg na kiungo wa kati wa Marekani Brenden Aaronson, 21, amekataa kuhusishwa na kuhamia Leeds United. (Yorkshir Post)

0 comments:

Post a Comment