Mechi ya robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika inayotarajiwa kuchezwa Jumapili katika Uwanja wa Olembe uliopo mji mkuu wa Cameroon, Yaoundé, imehamishwa.
Haya yanajiri baada ya watu wanane kufariki siku ya Jumatatu kufuatia msongamano nje ya uwanja kabla ya mechi kati ya Cameroon na Comoro.
Wawili kati ya waliouawa ni watoto wenye umri wa miaka sita na 14 na kadhaa walijeruhiwa.
Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf) Patrice Motsepe alisema mabadiliko kadhaa yanaendelea na mchezo wa Jumapili sasa utafanyika kwenye Uwanja wa Ahmadou Ahidjo uliopo Yaoundé.
0 comments:
Post a Comment