Rais wa Shirikisho la soka Afrika (CAF) Patrice Motsepe ametoa salama za pole kwa ndugu jamaa na marafiki kutokana na kutokea kwa tukio kufariki kwa mashabiki 8 wa soka na 38 kujeruhiwa jana nje ya uwanja wa Olembe.

Tukio la kufariki kwa mashabiki nane limetokea jana kuelekea mchezo wa Cameroon vs Comoro inaelezwa kuwa kulikuwa na msongamano na kukanyagana kwa mashabiki walipokuwa wanataka kuingia uwanjani.



Motsepe ameeleza kuwa mchezo ujao wa January 30 wa robo fainali ya AFCON utaamishwa na kupelekwa uwanja wa Ahmadou Ahidjo Younde.

”Tunajukumu la kujua nini hasa kilitokea na tahadhari gani zichukuliwe ili tukio kama hili lisijirudie tena, wakati watu wanapoteza maisha yao lazima uwe na hasira na kuhitaji kujua kilitokea nini na kuhakikishiwa kuwa hakitotokea tena”>>> Patrice Motsepe

Mabadiliko hayo yanafanya ili kupisha uchunguzi lakini kamishna wa mchezo huo ripoti yake inasema kuwa Uwanja wa Olembe unaingiza mashabiki 60,000 ila hakuruhusu kujaza uwanja sababu ya kujikinga na Corona, kila mchezo wa AFCON 2021 sasa utakuwa unasimama dakika moja kuomboleza.