Mashabiki wa Liverpool na Manchester United wameambiwa kwamba kutakuwa na maafisa wengi wa polisi mjini Moscow wiki ijayo.
Klabu hizo za Ligi Kuu ya Uingereza
zote zina mechi za klabu bingwa Ulaya katika mji mkuu wa Urusi,Takriban
mashabiki 2,000 watasafiri kuelekea kaskasini magharibi ambapo
Liverpool itacheza dhidi ya Spartac Moscow siku ya Jumanne na United
ikikabiliana na CSKA Moscow siku ya Jumatano.
United imewaambia mashabiki wake
kutovaa rangi za klabu hiyo ama hata kutembea Moscow wakiwa peke yao
Liverpool inasema kuwa mamlaka ya Urusi inajua kwamba vilabu hivyo
viwili viko mjini Moscow wakati mmoja kwa hivyo maafisa wengi wa polisi
wanatarajiwa mahali popote ambapo mashabiki wa Liverpool na Manchester
United watakongamana. Ikiwemo katika maeneo ya malazi.
Mashabiki sugu wa Urusi waliwashambulia wenzao wa Uingereza mjini Marseille katika kombe la bara Ulaya 2016.
0 comments:
Post a Comment